SAMIA: UZEE DAWA, WATANGULIZI WANGU WAMEKUWA MSAADA KUFIKIA MAFANIKIO
Автор: Dar24 Media
Загружено: 2025-06-27
Просмотров: 82
Rais Samia Suluhu Hassan amesema misingi imara iliyowekwa na watangulizi imemuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kufikia mafanikio mbalimbali katika ujenzi wa Tanzania.
Ametumia fursa hiyo kuwashukuru watangulizi wake katika nafasi ya urais, akisema kutoka kwao alijifunza na misingi imara iliyomuwezesha kupatikana kwa mafanikio kwenye kipindi cha miaka minne.
Rais Samia ameyasema hayo leo Ijumaa, Juni 27, 2025 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 jijini Dodoma.
“Nikiri kwamba misingi yao na ushauri wao kwa wale niliobahatika kufanya kazi, wamenisaidia sana mimi binafsi pamoja na Serikali ninayoiongoza,” amesema Rais Samia.
Pia, ameeleza kufurahishwa na hatua ya viongozi hao kuwepo bungeni na kwamba, msaada wao wa kimawazo na ushauri umeendelea kumjenga katika uongozi wake.
“Hakika nimeamini kuwa wazee ni dawa na palipo na wazee hapaharibiki jambo, nawashukuru sana,” amesema Rais Samia.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: