UKWELI WA KIBANGA KUMPIGA MKOLONI SABABU NI HII HAPA WANANCHI WA KWACHAGA WAMEFUNGUKA NASI
Автор: Kipanga Media
Загружено: 2021-07-17
Просмотров: 3710
Hatimae nimefanikiwa kufika katika Kijiji cha Kwachaga Kata ya Kwachaga Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga eneo lenye historia kubwa ya mtu maarufu aliyejulikana kwa majina ya Ally Mwisusa (KIBANGA) aliyempiga mkoloni yapata miaka 1940 iliyopita.
Nilipofika katika Kijiji cha Kwachaga Wilayani Handeni nje ya Kanisa Anglikana Mt, Albano niliukuta mti mkubwa aina ya Mkwaju ambao nilielezwa na moja ya wazee wa Kijiji hicho kuwa ulitumiwa na wana Kijiji kufanya mikutano wakati huo walipoitishwa na (Jumbe) mtawala.
Kwa mujibu wa mazungumzo yangu na Mzee Frank Mbelwa mkazi wa Kijiji na Kata ya Kwachaga alisema alizaliwa mnamo mwaka 1935 katika Kijiji hicho na mwaka 1942 wakati mzee Kibanga anampiga mkoloni yeye alishuhudia tukio hilo akiwa bado Kijana mdogo.
“Wakati huo Kibanga nilimuona akiwa Mzee wetu hapa Kijijini na Huyo Mkoloni nilimuona alikuwa akijulikana kwa jina la Pina yeye alikuwa bwana shamba alikuwa anakagua mashamba ya mihogo hapa Kijijini akiona shamba halijastawi anakasirika na kucharaza bakora”
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: