TUMEVUNJA, KUDHOOFISHA MITANDAO YA WAUZA DAWA ZA KULEVYA - RAIS SAMIA
Автор: Dar24 Media
Загружено: 2025-06-27
Просмотров: 195
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema vita dhidi ya matumizi na wauzaji wa dawa za kulevya imekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.
Amesema ndani ya uongozi wake, Serikali imeimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kupunguza uingizaji, usambazaji na uzalishaji wa dawa hizo ili kulinda afya za Watanzania hasa vijana.
Rais Samia ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma leo Ijumaa Juni 27, 2025 wakati akilihutubia Bunge ikiwa ni sehemu cha mkachakato wa kuhitimisha Bunge la 12.
“Katika kipindi hiki tumepambana kwa nguvu sana na wauza dawa za kulevya, tumedhoofisha mtandao wa uingizaji, uzalishaji na hata watumiaji. Tumekamata jumla ya kilo milioni 4.9 zikihusishwa watuhumiwa zaidi ya 25,000.
“Katika kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya Serikali imeongeza vituo vya huduma za tiba kwa warahibu wa dawa za kulevya kutoka vituo tisa mwaka 2020 hadi 18 mwaka 2025,” amesema Rais Samia.
Pamoja na mipango hiyo, Rais Samia amesema Serikali itaendelea kudhibiti na kuwalinda vijana dhidi ya dawa za kulevya.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: