WAFANYABIASHARA WA KWA MCHINA WAPAZA SAUTI KUHUSU MARUFUKU YA KUTUMIA MAENEO YA NJE YA MADUKA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2025-12-11
Просмотров: 1891
Wafanyabiashara wa eneo la Kwa Mchina wameiomba Serikali ya Zanzibar kupitia mamlaka husika kuangalia upya uamuzi wa kuwakataza kuweka bidhaa na kuendesha biashara katika maeneo ya nje ya maduka.
Wakizungumza na waandishi wa habari, wamesema maduka waliyokodisha yalikuwa na maeneo ya ziada mbele ya majengo ambayo yaliwasaidia kuonyesha bidhaa na kuwavutia wateja, bila kuathiri barabara au kuzuia njia za watembea kwa miguu. Wameeleza pia kuwa walihakikisha mitaro na maeneo ya umma yanabaki wazi kwa matumizi.
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa Baraza la Manispaa ya Mjini, Ghaitha Mzee, amesema hatua ya kuzuia matumizi ya maeneo ya nje ya maduka imetekelezwa kufuatia maagizo ya Serikali Kuu kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
#AsamOnlineTV #HabariZaLeo #ZanzibarUpdates #Biashara #Manispaa #YouTubeTrending
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: