Ufugaji wa Kondoo wa Dorper Kenya | Kamasi kwa Dorper Wapya na Ushauri wa Daktari
Автор: KILIMO NA LIMO
Загружено: 2026-01-18
Просмотров: 59
Karibu kwenye Ufugaji wa Kondoo wa Dorper Kenya.
Katika video hii, nashiriki tukio halisi lililotokea siku ya pili baada ya kuleta Dorper wangu wapya shambani. Asubuhi niligundua kamasi (runny nose) kwa baadhi ya Dorper, hali iliyohitaji hatua ya haraka.
Bila kuchelewa, niliamua kumpigia daktari wa mifugo mara moja, ambaye alifika shambani, akawakagua kondoo na kuwadunga dawa ya minyoo kwa sindano kama hatua ya awali ya matibabu na kinga.
Baada ya matibabu, nilifanya mahojiano na daktari wa mifugo ambapo anaeleza:
– Sababu zinazoweza kusababisha kamasi kwa kondoo
– Dawa aliyotumia na kwa nini alichagua injectable
– Ushauri muhimu kwa wafugaji wa Dorper wapya
– Umuhimu wa uangalizi wa afya kwa kondoo wapya
Video hii ni sehemu ya safari yangu ya kuanzisha mradi wa Dorper, ambapo nashiriki kila hatua kwa uhalisia — mafanikio, changamoto na maamuzi ya shambani.
Kama unapanga au tayari una ufugaji wa kondoo wa Dorper, video hii itakusaidia kujua nini cha kufanya haraka unapokutana na dalili za afya.
🔔 Subscribe, bonyeza like, na uwashe notifications utembee nami katika safari hii ya Dorper hadi kuwa biashara kamili.
#UfugajiWaDorper
#DorperKenya
#DorperFarming
#KondooWaDorper
#UfugajiWaKondoo
#DorperNiBiashara
#DorperKiswahili
#KilimoBiashara
#UfugajiKenya
#DorperJourney
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: