Bwana Yesu amevunja minyororo ya maovu (42 NW)
Автор: Shem Kabanza
Загружено: 2020-06-27
Просмотров: 15469
Bwana Yesu amevunja
minyororo ya maovu
42 NYIMBO ZA WOKOVU
1. Bwana Yesu amevunja
minyororo ya maovu,
nimewekwa huru kweli
mbali na makosa yangu.
Haleluya, haleluya!
Yesu Kristo ni Mwokozi!
Haleluya, haleluya!
Yesu alinikomboa.
2. Nilipoungama dhambi,
nikawekwa huru kweli.
Moyo wangu unawaka
kwa upendo ‘takatifu.
3. Kamba zilizonifunga
zimetoka, nafurahi.
Dhambi zilizo ‘sumbua
zimetupwa mbali sana.
4. Ninataka kuhubiri:
Nimewekwa huru kweli.
Nipeleke kwa furaha
neno zuri la Mwokozi
#Nyimbozawokovu
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: