Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

Mahubiri ya Baba Askofu Dkt. Isack Kisiri Laiser, Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Magharibi Kati, Tabora

Автор: KKKT DKMS Online TV

Загружено: 2025-04-06

Просмотров: 2016

Описание:

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amemtambulisha rasmi Msaidizi wa Askofu (Dean Mteule) Mch. Frank Richard Mntangi kwa washarika wa Kanisa Kuu Lushoto na wanadayosisi kwa ujumla huku wengine waliotambulishwa ni pamoja na Wakuu wa Majimbo yote 6 ya KKKT-DKMs pamoja na wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu ya KKKT-DKMs wanao wakilisha Jimbo la Kusini.

Askofu Dkt. Mbilu amefanya utambulisho huo kwenye Ibada ya Jumapili ya leo tarehe 6/4/2025 katika Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto kwakuwa Dean Mteule Mntangi ndiye atakayekuwa Mchungaji kiongozi wa Kanisa Kuu.Askofu Dkt. Mbilu pia amewataka wanadayosisi kuwapa ushirikiano viongozi hao ili waweze kutimiza vyema kazi ya Mungu waliyoitiwa.
Pia amemshukuru Dean Michael Kanju kwa kazi nzuri aliyoifanya katika Kanisa la Mungu.Dean Kanju amemaliza muda wake wa kutumika katika Ofisi ya Msaidizi wa Askofu pamoja na kufikisha muda wa kustaafu na hivyo tarehe ya Ibada ya kuagwa rasmi na kupewa heshma kwa Ibada maalumu ya Kustaafu kwa heshima itatajwa hapo baadae.

Mchungaji Frank Mntangi alithibitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tano (5) baada ya Jubilee yamiaka 125 ya Injili KKKT-DKMs uliofanyika KOTETI Magamba tarehe 03-05/2025,ambapo pia Mch. John Ndimbo alichaguliwa kuwa Mkuu wa Jimbo la Tambarare, Mch. Issai Mweta alichaguliwa kuwa Mkuu wa Jimbo la Pwani, Mch. Ishmael Ngoda, alichaguliwa kuwa Mkuu wa Jimbo la Magharibi, Mch. Anderson Kipande, alichaguliwa kuwa Mkuu wa Jimbo la Kusini, Mch. Charles Kakai, alichaguliwa kuwa Mkuu wa Jimbo Mteule wa Jimbo la Kaskazini na Mch. Tumaini Kallaghe yeye anaendelea kutumika katika Jimbo la Diaspora linalowahudumia Wakristo wanaoishi Uingereza na nchi jirani za Ulaya kama vile Ujerumani, Sweden, Denmark, Norway pamoja na Marekani. Makao Makuu ya Jimbo hili yapo Reading, Uingereza (UK).

Baba Askofu Dkt. Isack Kisiri Laiser, Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Magharibi Kati, Tabora ndiye aliyehubiri katika Ibada hii ambaye pia alishiriki Mkutano Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na alikuwa mnenaji Mkuu wa Mkutano huo na alipata nafasi ya kulifafanua vizuri neno Kuu la Dayosisi la mwaka 2025 kwa wajumbe wa mkutano huo.Neno kutoka kitabu cha Kutoka 33:14 "Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha".
Askofu Leisar, katika mahubiri amewataka wakristo kusimama kwenye Imani ya Yesu Kristo na kuwa tayari kupinga mafundisho potofu na huku akiwataka kusonga mbele kuendelea kumtumikia Mungu na kulijenga Kanisa lake kwa uaminifu mkubwa.

Ameongeza kuwa "Kanisa na Mwenye kanisa ambaye ni Bwana Yesu Kristo hahitaji longo longo kwani sio kama mama mkwe,anahitaji kutumikiwa kwa uaminifu na hakuna aliyewahi kushindana na Kanisa akapona" Ameongeza kuwa, kama Walutheri tushike neno la Mungu kikamilifu na tumuombe atusaidie kubadilisha wale wenye akili za hovyo wanaochafua Kanisa na kupotosha Neno la Mungu awarudishie akili zao na neno la Kristo likihubiriwa vizuri hata mawazo na fikra zao zitabadilika na wataacha longolongo zao.

Amewakumbusha pia Wachungaji,Wainjilisti na Waumini kufanyakazi kwa bidii na kuacha kuwa ombaomba,wakishatoka kuhubiri Injili waende kufanyakazi ili kujiepusha kufanya mambo ya hovyo.
huku akisisitiza kuwa sifa ya mwanaume katika familia sio kuvaa suruali na kuongeza watoto bali ni kuitunza familia yake hivyo ni wajibu wao kufanyakazi kwabidii ili waweze kukidhi mahitaji ya familia zao na hata wakinamama wasiwategemee tu waume zao kuhudumia familia bali pia wao wawe mstari wa mbele kushirikiana na waume zao katika kufanyakazi kwa maendeleo mazuri ya familia.

Mahubiri ya Baba Askofu Dkt. Isack Kisiri Laiser, Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Magharibi Kati, Tabora

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

IBADA YA SIKU YA PILI YA KRISMASI : 26/12/2025

IBADA YA SIKU YA PILI YA KRISMASI : 26/12/2025

Sehemu ya salamu za Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto.

Sehemu ya salamu za Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto.

SEHEMU YA PILI: Ibada ya kustaafu kwa heshima ya mchungaji Elinisa Shisaeli Kimaro

SEHEMU YA PILI: Ibada ya kustaafu kwa heshima ya mchungaji Elinisa Shisaeli Kimaro

Usimnyooshe Mtu Kidole | USIHUKUMU | Rev. Dr. Eliona Kimaro

Usimnyooshe Mtu Kidole | USIHUKUMU | Rev. Dr. Eliona Kimaro

IBADA YA KUWEKWA WAKFU NA KUINGIZWA KAZINI ASKOFU MTEULE DKT. DANIEL MONO  | 13/07/2025

IBADA YA KUWEKWA WAKFU NA KUINGIZWA KAZINI ASKOFU MTEULE DKT. DANIEL MONO | 13/07/2025

BABA ASKOFU LUDOVICK J. MINDE APIGA JEMBE NA KUBARIKI ENEO LA KUJENGA SHULE YA MSINGI

BABA ASKOFU LUDOVICK J. MINDE APIGA JEMBE NA KUBARIKI ENEO LA KUJENGA SHULE YA MSINGI

Sehemu ya Mahubiri ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, Usharika wa Soni, Mtaa wa Kwang‘wenda

Sehemu ya Mahubiri ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, Usharika wa Soni, Mtaa wa Kwang‘wenda

ASKOFU Dkt. HOTAY:

ASKOFU Dkt. HOTAY: "UTAMJUA MTU KWA MAMBO MAKUBWA MATATU...."

MATUKIO MATATU MAKUBWA YALIYOIBUA HISIA ZA WANAJIMBO LA KILIMANJARO KATI  NA BABA ASK. DR. F. SHOO

MATUKIO MATATU MAKUBWA YALIYOIBUA HISIA ZA WANAJIMBO LA KILIMANJARO KATI NA BABA ASK. DR. F. SHOO

REV. DR. ELIONA KIMARO: USHUHUDA WA 'HOUSEGIRL' ALIYEKUJA KUWA PROFESA

REV. DR. ELIONA KIMARO: USHUHUDA WA 'HOUSEGIRL' ALIYEKUJA KUWA PROFESA

🔴#LIVE:DKT.MBUNDA AIBUKA NA MAZITO KILICHOTOKEA OKTOBA 29/AMTAJA LISSU NA HATMA YA WASOMI KWENYE....

🔴#LIVE:DKT.MBUNDA AIBUKA NA MAZITO KILICHOTOKEA OKTOBA 29/AMTAJA LISSU NA HATMA YA WASOMI KWENYE....

Salamu za Naibu Katibu Mkuu wa Missioni na Uinjilisti wa KKKT Mch Godfrey Walalaze

Salamu za Naibu Katibu Mkuu wa Missioni na Uinjilisti wa KKKT Mch Godfrey Walalaze

IBADA YA SIKU YA KUKUMBUKA KUZALIWA KWA MWOKOZI YESU KRISTO 25/12/2025

IBADA YA SIKU YA KUKUMBUKA KUZALIWA KWA MWOKOZI YESU KRISTO 25/12/2025

Mahubiri  Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto.

Mahubiri Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto.

#ՈՒՂԻՂ. Դատապարտված է. 2026-ին Փաշինյանին ծանր ժամանակ է սպասվում. Հայկ Նահապետյան

#ՈՒՂԻՂ. Դատապարտված է. 2026-ին Փաշինյանին ծանր ժամանակ է սպասվում. Հայկ Նահապետյան

Waumini KKAM Kyela Wapinga Kuhamishwa Mchungaji Wao

Waumini KKAM Kyela Wapinga Kuhamishwa Mchungaji Wao

Շահումյան․ 20-րդ դարի ամենահակասական հայ կերպարը — Լենինի ժառանգ՞, թե Առաջին Հանրապետության թշնամի՞

Շահումյան․ 20-րդ դարի ամենահակասական հայ կերպարը — Լենինի ժառանգ՞, թե Առաջին Հանրապետության թշնամի՞

Mungu Atakufurahisha / Rev. Dr. Eliona Kimaro

Mungu Atakufurahisha / Rev. Dr. Eliona Kimaro

IBADA YA JUMAPILI KANISA KUU LUSHOTO 06/04/2025

IBADA YA JUMAPILI KANISA KUU LUSHOTO 06/04/2025

UFUNGUZI WA MKUTANO WA WACHUNGAJI  17 DECEMBER 2025

UFUNGUZI WA MKUTANO WA WACHUNGAJI 17 DECEMBER 2025

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]