IJUE HISTORIA YA JINA KAWE, TANGANYIKA PACKERS-DAR ES SALAAM MPAKA KUWA KANISA LA MWAMPOSA
Автор: PNTV Kiswahili
Загружено: 2025-03-11
Просмотров: 136
Tanganyika Packers LTD, Kawe, Dar es Salaam 1945-1975. Kilikuwa kiwanda cha kuchakata na kusindika nyama kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.
Eneo lote la Mloganzila (Muhimbili) lilikuwa ni eneo la Tanganyika Packers na ndilo eneo lililokuwa linatumika kuwapokea na kunenepeshea ng’ombe
Walipoletwa kutoka mikoani kwa treni wakiteremshwa stesheni ya Pugu, baada ya mwezi wanaswagwa kupelekwa Kawe kuchinjwa na kuchakatwa.
Kutoka Mloganzila kwenda kilipo kiwanda wakati wa kuswagwa, waingereza waliita COWS WAY (njia ya ng’ombe). Waswahili wakashindwa na kuita “KAWE”
Tanganyika Packers (TPL) kilikuwa kiwanda kikubwa, kikisindika nyama za kusaga kwenye makopo na kusafirisha nje mpaka kwa malkia wa Uingereza,
Kilikuwa kiwanda tanzu cha shirika la LEMCO (Liebig’s Extract of Meat Corporation) linalofadhiliwa na Uingereza, ambalo lilianzia miaka ya 1860 Uruguay.
Liebig ni heshima ya baba wa (Organic Chemistry), Justus von Liebig. Jengo la machinjio la LEMCO lipo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO.
Sehemu kubwa ya nyama kutoka Tanganyika Packers iliuzwa Ulaya hususani katika nchi ya Uingereza. Watanganyika walipata ajira katika kiwanda hicho.
Kiwanda cha Tanganyika Packers kilijengwa na wakoloni kutoka Uingereza 1945 na kilitoa zaidi ya ajira 2,500 ambapo 1,200 zilikuwa ni ajira za kudumu.
Walifanya kazi kwa shift, walichukuliwa kwa mabasi kazini. 1975 serikali ilikitaifisha kutoka kwa waingereza kuingia serikalini kufuatia sera za ujamaa.
Kiwanda cha TPL kilizalisha nyama za mabuchani, mafuta ya kutengeneza sabuni, damu ilikaushwa na mifupa ilisagwa na kuwa chakula cha kuku,
Pembe na kwato za ng’ombe zilichemshwa kwenye boiler zikatoa gundi, kiwanda pia kilisindika nyama na maharage kama ox-tail beans, ngozi nk
Katika vita ya Kagera 1978-1979, kiwanda kilitumika kuwalisha wapiganaji vitani. Chakula cha kusindika kilitoka kiwandani kwenda uwanja wa vita.
Mwaka 1975 Serikali ya Mwl, J.K. Nyerere ilitaifisha kiwanda cha Tanganyika Packers na kukifanya kuwa mali halali ya Serikali ya Tanganyika.
Baada ya Serikaki kutaifisha kiwanda, uzalishaji na ubora wa nyama iliyosindikwa ulipungua kwa kiasi kikubwa sana kwa kukosa utaalam na ufundi.
Serikali walinyimwa leseni ya kusafirisha nyama iliyosindikwa. Walinyimwa (phytosanitary certificate) kuthibitisha ubora wa vyakula vya package
Waingereza wakawanyima cheti cha ubora na usafi wa nyama inayozalishwa. Soko la Ulaya ambako ndiyo walikuwa wanunuzi wakubwa likapotea.
Soko la ndani likawa gumu kiwanda kikaanza kusambaza nyama zake kwenye mabucha ya ndani ya Dar es Salaam na baadae kiwanda kikafariki 1993
Taratibu kiwanda cha Tanganyika Packers kikaanza kufariki. Baadaye kilibinafsishwa kwa mbunge wa Kawe, hata hivyo aliishia kuuza mashine na vipuri.
Mbunge wa Jimbo la Kawe wakati huo alitokana na CCM, aliitwa Zainuddin Adamjee. aliposhindwa Kukiendeleza akaamua kung’oa mitambo na vipuri.
Mapaa, madirisha, milango na vifungashio vilipelekwa Mapambano (veterinary) na kupimwa kama vyuma chakavu na mapaa kuuzwa kama used.#mwaposa#arisechurchriverside
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: