TRILIONI 1.3 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KATAVI.
Автор: KATAVI RS
Загружено: 2025-07-05
Просмотров: 171
Mkoa wa Katavi Umepokea Jumla ya Tsh Trilioni 1.345 ajili ya shughuli za kukuza uchumi pamoja na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuboresha maisha na ustawi wa Jamii sambaba na utawala bora na uwajibikaji ndani ya Mkoa.
Taarifa ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, aliyoitoa leo Julai 5, 2025 wakati wa tamasha la Samia Day lililofanyika maalumu kwa ajili ya kumpongeza na kumshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma za kijamii mkoani hapa
Fedha hizo ni kwa ajili ya kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo hadi 2025, Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Mikakati mbalimbali ya Serikali.
Kufuatia utekelezaji huu wa miradi ya maendeleo timu ya vijana wa Dejong kutoka Kizimkazi Zanzibari wamefika ili kujionea namna ambavyo miradi hii imekuwa na msaada kwa jamii na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Mratibu wa timu hiyo Hassan Hamdu akizungumza na wananchi katika tamasha hilo amesema ujio wao umelenga kuwaonyesha wananchi wa mkoa wa Katavi umuhimu wa uwepo wa miradi mikubwa ya kimkakati katika jamii hususani katika nyaja za afya, Elimu, Uchumi, usafirishaji pamoja na miradi mingine.
"Tumejionea miradi mikubwa ilitekelezwa na serikali ya awamu ya sita, itoshe kusema serikali imenuia kuondoa kero ambazo awali zilikuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya wananchi, huduma za afya zimeboreshwa na sasa huduma za kibingwa zinapatikana hapa hapa Katavi na kwa bei nafuu," amesema Hamdu.
Aidha amesema katika upande wa elimu ni Fursa kwa wananchi kuweza kutumia miundombinu iliyopo kwa watoto kupata nafasi kusoma na kufikia malengo ya serikali ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. mwanamvua Mrindoko akizungumza katika tamasha hilo amesema hadi kufikia Juni, 2025 Mkoa una jumla ya Shule za Msingi 293, ambapo kati ya hizo za Serikali ni 278 na zisizo za Serikali ni 15. Mkoa una Shule za Sekondari zipatazo 79 zikiwemo 74 za Serikali na 5 ni Shule za binafsi, Sekta ya Elimu imepokea kiasi cha Sh Bilioni 58.093 zilizotumika katika kuboresha miundombinu ya Shule mbalimbali na kuweka mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunza
Mhe. Mrindoko Ujenzi wa Shule mpya 137 zikiwemo Shule 97 za Msingi na Shule 40 za Sekondari, madarasa 2,219 madarasa ya awali 6, matundu ya vyoo 2,734 hali ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa umbali wa kutembea kwenda Shule na msongamano wa Wanafunzi madarasani na kuwezesha mazingira bora zaidi kwa Walimu na Wanafunzi.
Mwisho
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: