Ask. Bagonza afiwa na Dada yake siku moja baada ya kumzika Baba yake.
Автор: ELCT-KARAGWE DIOCESE
Загружено: 2025-09-29
Просмотров: 17990
Baba Askofu Dr. Benson Kalikawe Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, kwa niaba ya familia ya hayati Benjamini Yakobo Bagonza; anatoa shukrani nyingi kwa wote mlioungana na familia yao kumsindikiza baba yao kwa mazishi yaliyofanyika tarehe 27/09/2025. Mungu awabariki sana.
Pamoja na shukrani hizo, anapenda kuwatangazia tena, kifo Cha dada yake DORA BAGONZA, ambaye ni kifungua mimba wa baba na mama yao mzazi; kilichotokea tarehe 28/9/2025, saa 12.45 asubuhi, katika Hospitali ya Regency - Dar es salaam. Mwili utasafirishwa kuja Karagwe tarehe 29/9/2025 na mazishi yatafanyika nyumbani kwao Irundu - Nyakahanga, Karagwe; siku ya Jumanne, tarehe 30/9/2025, kuanzia saa 3.00 asubuhi.
Habari ziwafikie ndugu, Jamaa na marafiki wote, popote walipo.
"...Alitoa, Ametwaa...Hatutamuwazia Mungu kwa upumbavu" Ayubu 1:21-22
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: