KANISA LA BIL 2.26 KWA MIKONO YA WAUMINI WA KKKT MAJENGO LAZINDULIWA
Автор: TZA MEDIA HUB
Загружено: 2025-07-20
Просмотров: 1570
K
Katika kile kinachotajwa kuwa ni ushindi wa kiroho, mshikamano na moyo wa kujitolea, waumini wa Usharika wa Majengo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini wamefanikiwa kukamilisha jengo la ibada la kisasa lenye thamani ya shilingi bilioni 2.26 bila msaada wowote kutoka kwa wafadhili wa nje.
Jengo hilo, ambalo lina uwezo wa kuchukua waumini 1,200 kwa wakati mmoja, limezinduliwa rasmi katika ibada ya Dominika ya Tano baada ya Utatu, iliyoongozwa na Askofu Mkuu Mstaafu wa KKKT, Dkt. Fredrick Shoo.
Akizungumza wakati wa ibada hiyo, Dkt. Shoo alisifu uamuzi wa washarika kujitegemea katika kugharimia ujenzi huo, akisema ni mfano adimu unaopaswa kuigwa na makanisa mengine.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: