RC MALISA AWATUMIA UJUMBE WAFANYABIASHARA WA JIJI LA MBEYA/ KATENI NA HUISHENI LESENI ZANU
Автор: Site Tv Online
Загружено: 2025-10-25
Просмотров: 107
SAUTI YA RC MALISA KWA WAFANYABIASHARA WA JIJI LA MBEYA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Beno Malisa amewataka wafanyabiashara Mkoani humo kuendeleza Utaratibu wao kulipa Kodi Kwa kukata na kuhuisha leseni zao na kusisitiza kuwa Kodi hiyo haimnufaishi Kiongozi yeyote wa serikali badala yake hutumika kwaajiri ya kujenga na kuboresha miundombinu ya Miradi ya Maendeleo.
Malisa amewaeleza wafanyabiashara kuwa kile wanachokichangia Kwa kukata leseni zao na kuhuisha hakitumiki tofauti badala yake kinakwenda kuboresha miundombinu mbali mbali ikiwemo ya Afya na Elimu Kwa kununua vifaa tiba, vifaa vya Shule na kutengeneza Madawati na viti na meza kwaajiri ya Wanafunzi.
Ameyasema hayo Leo Oktoba 25 wakati akikabidhi Madawati Elfu Moja(1000) kwenye Shule za Msingi 15 na viti na meza 576 Kwa Shule za sekondari yaliyotrngrnezwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wao wa kutokomeza swala la Wanafunzi kukaa Chini.
Awali akitoa salamu za Wilaya Bi Devotha Chacha Afisa tawala Wilaya aliyemwakilisha Mhe. Mkuu wa Wilaya amesema kama Wilaya wameamua kumtua mzigo mzazi wa kuchangia gharama za kiti na meza au Dawati la mtoto wake badala yake aelekeze Nguvu katika kutafuta Riziki zingine za Familia.
Justice Kijazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya amesema Jumla ya Madawati yaliyotengenezwa ni zaidi ya Elfu Mbili(2000) licha ya kukabidhiwa Elfu Moja na ameweka bayana kuwa yote haya ni sehemu ya utekelezaji wa Maelekezo ya serikali kuhakikisha makusanyo yanayokusanywa yanatekeleza Miradi ya Maendeleo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: