Babalevo akabidhiwa Ambulance mpya kwaajili ya Kigoma Mjini naomba sana Itunzwe 'Mimi ni chawa wa..'
Автор: SamMisago
Загружено: 2025-11-29
Просмотров: 1225
Leo, Novemba 29, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, @officialbabalevo, amepokea gari mpya ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa niaba ya wananchi wa Kigoma Mjini.
Ambulance hiyo imekabidhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Maweni, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya afya nchini.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Baba Levo amewaomba wananchi pamoja na watumishi wa hospitali hiyo kutunza na kuitumia ambulance hiyo kwa uadilifu na weledi ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi wote wanaohitaji msaada wa dharura.
Aidha, Mbunge huyo ameongeza kuwa Serikali ina mpango wa kuongeza magari mengine ya kubebea wagonjwa ifikapo mwaka ujao, ili kuendelea kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wa Kigoma Mjini na mkoa kwa ujumla.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: