JESHI LA POLIS LAANZA KUFANYA KAZI SAA 24 ENEO LA MLIMA LWAMBA,KUZUIA AJALI.
Автор: MWESI TV
Загружено: 2025-06-14
Просмотров: 30
KAMATI YA USALAMA BARABARANI MBEYA YAENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO YA MHE MKUU WA MKOA.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga ambaye pia ni Mlezi wa Kamati ya usalama barabarani Mkoani humo aliwaongoza wajumbe wa kamati hiyo kufanya ukaguzi wa maendeleo ya utekelezaji wa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Dkt Juma Homera.
Kamanda Kuzaga ameeleza kuwa kwa upande wa Jeshi la Polisi tayari limeanza kufanya kazi saa 24 katika eneo la Mlima Iwambi kwa kuweka kizuizi (barrier) pamoja na kuimarisha doria za Pikipiki kwa ajili ya kuzuia ajali na kutoa msaada wa haraka pindi inapotokea changamoto ya barabarani.
Aidha, Meneja wa Wakala wa Barabarani Mkoa wa Mbeya (TANROADS) Mhandisi Masige ameridhishwa na kasi ya maendeleo ya utekelezaji wa maelekezo kwani tayari mkandarasi yupo eneo la kazi, kazi ya kuweka taa za mwanga kwa ajili ya Askari watakaokuwa wakifanya ukaguzi inaendelea.
Aliongeza kuwa, tayari wameanza kuwalipa wakazi wa eneo la Mlima Iwambi ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo itakayoruhusu magari kupishana bila shida baada ya utanuzi.
Akiongea kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya usalama barabarani, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Rajabu Ghuliku amesema kuwa wameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa maelekezo kwa upande wa Jeshi la Polisi na Wakala wa Barabara kwani kukamilika kwa kazi hizo kutasaidia kupunguza ajali katika eneo la Mlima Iwambi.
Itakumbukwa Juni 08, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Dkt Juma Homera baada ya kukagua eneo la Mlima Iwambi ilipotokea ajali iliyohusisha magari matatu na kusababisha vifo na majeruhi alitoa maelekezo ya kujengwa kwa barabara ya mchepuko, Jeshi la Polisi kufanya doria saa 24 pamoja na kufungwa taa eneo la ukaguzi wa magari.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: