MAIGE, DIWANI ALIEMALIZA MUDA WAKE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUTETEA KITI CHAKE ZINGIZIWA
Автор: Kimeza Production
Загружено: 2025-06-28
Просмотров: 67
Diwani aliemaliza muda wake katika Kata ya Zingiziwa Ilala Dar es salaam, Mheshimiwa Maige Selemani Maganga, leo tarehe 28 Juni 2025, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania tena nafasi ya udiwani katika kata hiyo kupitia chama hicho.
Hatua hiyo imekuja baada ya kumaliza kipindi chake cha uongozi, na sasa anatarajia kupata fursa nyingine ya kuwatumikia wananchi wa Zingiziwa endapo atapitishwa na chama na kushinda katika uchaguzi ujao.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Mh. Maganga alieleza kuwa ana imani kubwa kuwa wananchi wa Zingiziwa bado wana matumaini naye kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo aliouongoza katika kipindi kilichopita.
Aliongeza kuwa ana nia ya dhati ya kuendeleza kazi aliyoianza kwa kushirikiana na wananchi na chama chake.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: