Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

TCCIA NA AGRA WABISHA HODI MTUKULA

Автор: TCCIA BUSINESS TV

Загружено: 2025-11-21

Просмотров: 88

Описание:

Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Hamisi Mayamba Maiga, amezindua rasmi mahema maalumu ya kuboresha mazingira ya biashara kwa vijana na wanawake katika mpaka wa Mutukula, mkoani Kagera. Mradi huo unatekelezwa na TCCIA kwa ushirikiano na AGRA, ukiwa na lengo la kukuza biashara za mpakani na kuongeza usalama wa shughuli za kiuchumi.
‎
‎Uzinduzi huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi unaoendelea katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo tayari umefanyika Kigoma na sasa umefika Kagera.
‎
‎Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Maiga aliipongeza TCCIA na AGRA kwa juhudi za kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, hususan vijana wanaojishughulisha na biashara za mazao, mboga mboga na matunda katika maeneo ya mipakani.
‎
‎“Kwanza nitoe pongezi sana kwa TCCIA na AGRA kwa kuandaa mradi huu na kuutekeleza kwa viwango. Hii ni fursa kubwa kwa vijana wetu, hasa hawa wa mpakani,” alisema.
‎“Serikali inaunga mkono jitihada hizi; endeleeni kuzifikisha katika mipaka yote nchini.”
‎
‎Aidha, aliwataka vijana na wafanyabiashara kutumia mahema hayo kama jukwaa muhimu la kupata taarifa za masoko, kuripoti changamoto zisizo za kikodi, na kuongeza ufanisi wa biashara zao.
‎
‎“Tumieni platform hii kutafuta taarifa, kutangaza bidhaa na kuripoti vitendo kandamizi ili mfanye biashara vizuri na mchangie ukuaji wa uchumi wetu,” aliongeza.
‎
‎Uzinduzi huo uliambatana na mafunzo ya Whistle Blowing kwa wafanyabiashara wa Mutukula, yaliyolenga kupambana na vizuizi visivyo vya kikodi (NTBs), kuripoti changamoto kwa njia za kidigitali, kuboresha ubora wa bidhaa na kutumia mitandao ya kijamii kupanua masoko.
‎
‎Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa TCCIA Kagera, Bw. Rwechungura Mali, alisema chemba hiyo itaendelea kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati kupitia mafunzo na kuwaunganisha na mitandao ya kibiashara. Aliwahimiza wafanyabiashara kujiunga na TCCIA ili kufungua fursa zaidi za ukuaji.
‎
‎Mradi huo unatarajiwa kuongeza ufanisi wa biashara mpakani, kuimarisha usalama wa bidhaa, kupunguza rushwa na gharama za uendeshaji, pamoja na kukuza uchumi wa vijana na wanawake. Utekelezaji wake katika mikoa ya Kigoma na Kagera tayari umeanza kuleta matokeo chanya.

TCCIA NA AGRA WABISHA HODI MTUKULA

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

MAFUNZO YA WHISTLE BLOWING YAONGEZA UWEZO WA WAFANYABIASHARA MIPAKANI

MAFUNZO YA WHISTLE BLOWING YAONGEZA UWEZO WA WAFANYABIASHARA MIPAKANI

JUKWAA LA WAANDISHI WA HABARI WALIVYOMBANA WAZIRI MKUU MWIGULU, TUMEPOTEZA UWAMINIFU KWA WANANCHI

JUKWAA LA WAANDISHI WA HABARI WALIVYOMBANA WAZIRI MKUU MWIGULU, TUMEPOTEZA UWAMINIFU KWA WANANCHI

Вы просыпаетесь в 3 часа ночи? Вашему телу нужна помощь! Почему об этом не говорят?

Вы просыпаетесь в 3 часа ночи? Вашему телу нужна помощь! Почему об этом не говорят?

ELIMU YA BIASHARA YAPAMBA MOTO KIGOMA; WASHIRIKI WAONA MWELEKEO MPYA WA UFANISI

ELIMU YA BIASHARA YAPAMBA MOTO KIGOMA; WASHIRIKI WAONA MWELEKEO MPYA WA UFANISI

HATUA BORA ZA UANDISHI, KATIKA UFANYAJI WA TAFITI   KAMISHNA DKT. IDD R. MANDI

HATUA BORA ZA UANDISHI, KATIKA UFANYAJI WA TAFITI KAMISHNA DKT. IDD R. MANDI

Simulizi ya mfanyabiashara aliyesababisha Waziri Mkuu kumsimamisha kazi ofisa wa TRA

Simulizi ya mfanyabiashara aliyesababisha Waziri Mkuu kumsimamisha kazi ofisa wa TRA

MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA WAIPONGEZA SERIKALI UJENZI WA SKANA MUTUKULA

MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA WAIPONGEZA SERIKALI UJENZI WA SKANA MUTUKULA

Madagascar : l'île aux richesses confisquées, jusqu'à quand ?  | Expliquez-moi...

Madagascar : l'île aux richesses confisquées, jusqu'à quand ? | Expliquez-moi...

'KATOENI ELIMU MASHAMBANI-RC MRINDOKO.

'KATOENI ELIMU MASHAMBANI-RC MRINDOKO.

TCCIA NA PACCI KUWEZESHA WANAWAKE BIASHARA ZA KIMATAIFA

TCCIA NA PACCI KUWEZESHA WANAWAKE BIASHARA ZA KIMATAIFA

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO KALI KUELEKEA DEC 9 KWA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO KALI KUELEKEA DEC 9 KWA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA

KAMISHNA  DKT. IDD MANDI AKIELEZEA KUHUSU SHERIA YA KUANZISHWA KWA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA

KAMISHNA DKT. IDD MANDI AKIELEZEA KUHUSU SHERIA YA KUANZISHWA KWA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA

Восьмиконечная звезда: от стен монастыря до флага Азербайджана / ХРОНИКА ЗАПАДНОГО АЗЕРБАЙДЖАНА

Восьмиконечная звезда: от стен монастыря до флага Азербайджана / ХРОНИКА ЗАПАДНОГО АЗЕРБАЙДЖАНА

Как мы живём в самом холодном городе мира — Экскурсия по типичной квартире Якутск, СИБИРЬ (-64°C ...

Как мы живём в самом холодном городе мира — Экскурсия по типичной квартире Якутск, СИБИРЬ (-64°C ...

KWASASA MABALOZI WOTE DUNIANI WANANGEA NA CHEMBA - RAIS WA TCCIA VICENT MINJA

KWASASA MABALOZI WOTE DUNIANI WANANGEA NA CHEMBA - RAIS WA TCCIA VICENT MINJA

Zrób to TERAZ, a Święta będziesz mieć z głowy! BIGOS Staropolski do SŁOIKÓW / Oddaszfartucha

Zrób to TERAZ, a Święta będziesz mieć z głowy! BIGOS Staropolski do SŁOIKÓW / Oddaszfartucha

jinsi ya kulipia malipo ya kampuni  kila mwaka TRA#TRA anual return#Tanzania revenue authority #TRA

jinsi ya kulipia malipo ya kampuni kila mwaka TRA#TRA anual return#Tanzania revenue authority #TRA

Я не знал, что ИРАН такой? Местная жизнь в Казвине меня удивила!

Я не знал, что ИРАН такой? Местная жизнь в Казвине меня удивила!

Уникальная немецкая кинохроника штурма Брестской крепости (1941)

Уникальная немецкая кинохроника штурма Брестской крепости (1941)

COPRA LINDI

COPRA LINDI

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]