HALMASHAURI YA MJI WA MBULU YAIBUKA KIDEDEA KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA PILI, NNE NA SITA 2024-2025
Автор: Come Tv Tanzania
Загружено: 2025-09-27
Просмотров: 359
Kuu wa Wilaya ya Mbulu, Mheshimiwa Michael Semindu, amewapongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Idara ya Elimu, pamoja na vyama vya walimu kwa mchango mkubwa uliowezesha halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya elimu mitihani ya kidato cha Pili, Nne na Sita mwaka 2024 - 2025. Pamoja na mafanikio hayo, Mheshimiwa Semindu alisisitiza umuhimu wa kushughulikia changamoto za kijamii ikiwemo ukatili wa kijinsia na udumavu wa watoto, huku akiipongeza pia Halmashauri ya Mbulu kwa kuongoza katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mheshimiwa Michael Semindu, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu pamoja na Idara ya Elimu kwa juhudi kubwa zilizowezesha halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza kitaifa. Vilevile, alivitambua vyama vya walimu kwa mchango mkubwa waliotoa katika sekta ya elimu.
Mkurugenzi wa Halmashauri, Mhe. Reheme Bwasi, alisema Mbulu imekuwa halmashauri ya kwanza kati ya halmashauri 184 nchini kwa vigezo vya Key Performance Indicators (KPI) vinavyotumika na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupima matokeo ya sekondari.
Kwa upande wa kidato cha pili, Mbulu ilishika nafasi ya tatu kitaifa kwa kufaulisha kwa asilimia 45 daraja la kwanza hadi la tatu.
Bwasi alieleza kuwa halmashauri hiyo ina shule 23 za sekondari, zikiwemo 18 za serikali na 5 binafsi, pamoja na vituo 11 vya kujitegemea. Jumla ya wanafunzi ni 12,079 na walimu 346, wakiwemo walimu 126 wa masomo ya sayansi na 220 wa masomo ya sanaa.
Mkurugenzi huyo alitoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha za uboreshaji wa elimu, pamoja na walimu, maafisa elimu na wadau mbalimbali kwa mchango wao mkubwa ulioiwezesha Mbulu kushika nafasi ya juu kitaifa.
Afisa Elimu Sekondari Bi. Elizabeth Lusingu, akizungumza amesema: Pamoja na kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, tume pokea maelekezo muhimu ambayo tutayafanyia kazi. Maelekezo haya yanahusu masuala ya kupambana na ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, kuboresha lishe na malezi ya watoto, pamoja na kusimamia malezi na maadili ya kazi. Kama ofisi ya elimu sekondari, tumejipanga kuhakikisha kwamba maelekezo haya yanasimamiwa ipasavyo katika halmashauri zote, ili kuimarisha utoaji wa huduma bora na kusaidia halmashauri zetu kuwa mfano wa kuigwa.
Mwalimu Faustin Suluhu Sanga, Mkuu wa Shule ya Sekondari Tlawi Mbulu,kwa niaba ya Walimu na wakuu wa taasisi za elimu amemshukuru mkuu wa wilaya ya mbulu Mhe. Michael Semindu kwa kuwatunuku vyeti vya pongezi kwa walimu na shule zilizofanya viziri kitaifa zaidi halmashauri yam ji wa mbulu kuwa ya kwanza kitaifa ambapo haijawai kutokea.
Hafla hiyo imeacha alama kubwa katika historia ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu, ikiwa ni uthibitisho wa mshikamano na juhudi za pamoja kati ya walimu, viongozi wa serikali na wadau wa elimu. Mbulu sasa imeweka rekodi mpya kitaifa na kuonesha kuwa ushirikiano wa kweli unaweza kubadili mustakabali wa elimu nchini.
@USTAWIWAJAMIITZ @Belitskay @mbulusfcommunity1966 @HanaG @hanangrini2145 @HereslifeMbulu @lettambulu1411 @RousseauMbulu @BINTANGMBULUSAN
Come Tv Tanzania
Mwandishi: Hussein Thabit
Eneo: Kata ya Sanu, Mbulu
Tarehe: 26.09.2025
#subscribe #share #like #comment
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: