HII NDIYO VIDEO ILIYOMPONZA LISSU NA KUJIKUTA AKIKAMATWA NA POLISI?
Автор: ITV Tanzania
Загружено: Premiered Apr 10, 2025
Просмотров: 178,759 views
#HABARI: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, alielezwa kukamatwa Jumatano, Aprili 09, 2025, mkoani Ruvuma, muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara uliokuwa sehemu ya kampeni ya chama chake ya "No Reforms No Election" na harambee ya kuchangia chama kwa jina la Tone Tone.
Taarifa rasmi kuhusu sababu ya kukamatwa kwake bado hazijatolewa na vyombo vya dola, lakini mjadala umeibuka mitandaoni miongoni mwa wachambuzi wa siasa na wananchi, wakihusisha tukio hilo na kauli aliyoitoa siku chache kabla ya tukio hilo.
Kauli hiyo, iliyotolewa Aprili 3, 2025, katika mkutano wa ndani wa CHADEMA wa kitaifa uliohudhuriwa na viongozi wa chama na watia nia wa ubunge kutoka majimbo mbalimbali nchini, inatajwa kuwa huwenda ni miongoni mwa sababu zinazochochea tafsiri Lissu kukamatwa.
ITV Digital tunaendelea kufuatilia sakata hili na tunaamini vyombo vya dola vitatoa taarifa rasmi na sababu za kumshikilia Lissu.
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ;
Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
Facebook : https://bit.ly/2KeQNl3
Twitter : https://bit.ly/2XG7aii
Instagram : https://bit.ly/34KItmg

Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: