SIMULIZI ZA MAJERUHI AJALI ILIYOUA 38 SAME, MABASI KUGONGANA, KUWAKA MOTO ABIRIA WAKIWA NDANI
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-06-29
Просмотров: 70686
Mudin Waziri ambaye ni majeruhi wa ajali hiyo aliyelazwa Hospitali ya mjini Same, amesema alikaa siti ya nyuma na wakati ajali inatokea alirushwa mbele na wakati huo kila mtu alikuwa anapambana kivyake kutoka ndani ya basi.
Majeruhi mwingine, miliad Mndeme amesema akiwa ndani ya basi la Chanel One tairi la mbele upande wa kushoto wa basi hilo lilipasuka na kugongana na gari lingine na kushika moto.
Akizungumza Mganga mfawithi Hospitali ya Mji wa Same, Dk Lwitiko Mwalukumba amesema miili minne kati ya mitano ambayo haikuungua sana imetambuliwa.
Naye, Mkuu wa Wilaya hiyo, Kasilda Mgeni amesema mabaki ya miili ya watu 33 imepelekwa hospitali ya KCMC kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya vinasaba (DNA) ili kuitambua.
Ajali hiyo iliyoua watu 38 na majeruhi 29, ilitokea Juni 28, 2025 katika eneo la Sabasaba, Same mjini ikihusisha basi kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na basi dogo aina ya coaster lililokuwa likitokea Same mjini kwenda Moshi kugongana uso kwa uso na kuungua moto wakati abiria wakiwa ndani ya magari hayo.
🎥 - Ombeni Daniel .
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: