Kimasomaso -Issa Matona
Автор: Zanzibar orchestra
Загружено: 2025-09-19
Просмотров: 6827
Aye masomaso mwanangu asimuone
Kimasomaso mwanangu asimuone
Kwa jicho la hasidi mwanangu asimuone
Ah na wambaya wetu eeh mwanetu asimuone
Masooo mwanangu asimuone
Hongera mwanangu eeh hongera
na mimi mamae tuhongere
Nasema yuwapi weeh
yuwapi mamae harusi aje hapa tuhangaike nae
nasema yuwapi jamani leo
yuwapi mama
Na mamae harusi namtaka aje hapa
Shangazi lake harusi nae namtaka aje hapa
Na dadaake harusi nae namtaka aje hapa
Na bibiake nae namtaka aje hapa
na somo yake harusi namtaka aje hapa
tuje tumfunze mwari asije kufedheheka
ukiitwa na mumeo mama wajibu kumuitika
ukiitwa ewe bibi uitike bwana labeka
umridhie mumeo mama kwa kila analotaka
ijapokuwa na mwao sitaki mnitukane
nnawaita wazazi waje hapa tuonane
wanipe mkaja wangu upatao mia nane
umuweke utangani mwari amsemeza aseme
uinue uso nyuma mama wahisani uwaone
uangaze kila pembe na wabaya uwaone
anapokuwa mumeo hujambo muulizane
uufungue mkoba mama kilo ndani ukione
utahadhari na shoga wasije wakunyang’anye
salkheri njiani wengine si wanaume
leo umepata wako mahawara na wakome
hodi hodi nnakuja kuja na langu shauri
mlombali msogee wala msitaakhari
makungwi mkusanyike imeingia hatari
vifunikavyo vyaliwa vinaachwa vilowazi
mwari amevunja ungo mutahadhari walezi
somo yake biharusi hebu nitafutieni
na kungwi lake harusi wote waje hapa uwanjani
tuje tumfunze mwari malezi ya kizamani
unapopelekwa kwako mama unapofika nyumbani
ukacheke na mumeo mama umpumbaze chumbani
wakaja na ndugu zako wakaribishe chumbani
wakaja mawifi zako mama uinuke kitandani
wanapokuja wakwezo uwaweke ukumbini
wakaja shemegi zako uwaweke barazani
wakaja mashoga zako sema nao dirishani
wakikuaga kwaheri uwambie karibuni
ufunge mlango wako urejee kitandani
huku ukichekacheka na macho yawe laini
nasema na dada zangu nyie mnaokaa mjini
nyie mnao waume leo sikizeni kwa makini
karandinga limelia vibaibui begani
muwazuwie waume wasirande majiani
muwafunge kwa vitanzi muwafiche maziwani
akija akikutoka mume humuoni asilani
atapikiwa mkate na vichuzi bakulini
atafukizwa na udi na asumini kitandani
atakupita na honda yule sie bwana khalfani
utolewe kwate lako ulie na mito kitandani
ndugu zangu maharusi sikizeni nnasema
tumengia mitamboni watu wote wanaona
wazazi wa mke na mume wote wamekusanyana
huu ni wangu wasia msiseme natukana
mashoga wa siku hizi ujue hawana maana
mkikutana njiani eti hujambo huulizana
utamfanya mpenzi siri zenu kupeana
umkaribishe njiani furaha na taadhima
utampikia dhifa nyingi nyingi zilonona
umuoneshe wazazi huyu baba huyu mama
ukimuonesha shemegi atamwinukia wima
atafanya kila mbinu apate kumuandama
fadhila na ihisani hatozikumbuka tena
akuache unalia njiani unalalama
utatamani akhera nawe ungali mzima
kama atakwita bibi nimekuzalia nani
miezi miwili mitatu mama mibegi yako kichwani
huu ni wangu wasia Issa nnasema uwanjani
sikizeni kwa makini nyie wari mlovipembni
ukaisikia hodi mama ushungi uwe kichwani
huenda akawa mumeo mama usimkere moyoni
kama ndie bwana pita kwa sauti ya huzuni
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: