VIJANA WAMETAKIWA KULIHESHIMISHA TAIFA / TUNAWATEGEMEA
Автор: One Step Mediatz
Загружено: 2025-04-11
Просмотров: 19
VIJANA ACHENI HAYA TAIFA LINAWATEGEMEA
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua, amewasihi vijana kujiepusha na mambo yote yanayoweza kuwafanya wasiwe tegemeo kwa familia zao, jamii na Taifa, akibainisha baadhi ya mambo hayo kuwa ni rushwa, madawa ya kulevya na ukatili.
Dkt. Chuachua ametoa nasaha hizo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi ya vijana wa kujitolea OP miaka 60 ya Muungano, katika kikosi cha jeshi 821KJ Bulombora wilayani Kigoma, ambapo amewapongeza vijana kwa kufikia hatua hiyo muhimu ya kuhitimu mafunzo hayo.
Nasaha hizo za Mkuu wa Wilaya zimetanguliwa na salaam kutoka kwa Kanali Juma Mrai, akimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele na Brig. Jen. Anna Mkinga, akimwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo.
Baadhi ya wazazi wa vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi wamelishukuru Jeshi la Kujenga Taifa JKT, kwa kuwapatia mafunzo ya ukakamavu na kuwalea kimaadili watoto wao, huku baadhi ya vijana wahitimu wakieleza machache kati ya mengi waliyovuna kipindi chote cha mafunzo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: