VIKUNDI VYAASWA KUREJESHA MIKOPO KWA WAKATI
Автор: Radiojamii Kilosa
Загружено: 2025-12-02
Просмотров: 67
Vikundi mbalimbali Wilayani Kilosa vimeaswa kurudisha mikopo waliyokopa kwa wakati ili iweze kuwasidia na watu wengine wanaohitaji mikopo hiyo.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka kwenye halfa ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 awamu ya pili ya Halmashauri kwa ajili ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri Jumatatu 1, Desemba 2025.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Shaka amesema kumekuwa na changamoto ya urejeshwaji wa marejesho ya mikopo hiyo, hivyo amevitaka vikundi vikatumie mikopo hiyo kwenye malengo yalikusudiwa kwani itawasidia kunyanyuka kiuchumi na kufanya marejesho kwa wakati.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: