Nimefika kwake Yesu ( 35 NW )
Автор: Shem Kabanza
Загружено: 2020-05-12
Просмотров: 159191
https://www.nyimbozawokovu.online/35-...
35 Nimefika kwake Yesu
Nyimbo Za Wokovu
#Nyimbozawokovu
1. Nimefika kwake Yesu,
Na rohoni mwangu sasa,
jua lake la neema
linang’aa kila siku.
Pambio:
Roho yangu inaimba,
nimefunguliwa kweli.
Nimekaribia Yesu,
ninaimba kwa furaha.
2. Pepo za neema yake
zinavuma ndani yangu,
na mawimbi ya wokovu
yananijaliza sasa.
3. Sasa Bwana Yesu Kristo
amefanya kao kwangu.
Nimepewa mfariji,
Roho ya ahadi yake.
4. «Siku roho afikapo
mtajua kwa hakika
kwamba ninakaa kwenu»,
hivyo Yesu alisema.
5. Kweli, amefika kwetu,
sasa yumo ndani yetu.
Ujitoe kwake Mungu,
aioshe roho yako!
6. Yesu atakapokuja
katita utakatifu,
nitafananishwa naye,
nitamshukuru sana.
Pambio 2:
Zitakuwa nyimbo nyingi
tuta’poingia mbingu,
na milele tutaimba
na kusifu Mungu wetu.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: