Jinsi Ya Kupika Dagaa Watamu
Автор: Misosimitamu
Загружено: 2025-11-06
Просмотров: 1703
Viungo
• Mafuta – 2 tbsp
• Kitunguu – 1 medium, kimekatwa
• Ginger-garlic paste – 1 tbsp
• Dagaa (samaki wadogo waliokaushwa) – 300g, tayari kukaangwa
• Nyanya – 2, zimekatwa
• Tomato paste – 1 tsp
• Chumvi – ½ tsp
• Lemon juice – 1 tbsp
• Maggi – 1 tsp
• Fish masala – 1 tsp
• Karoti – 1, imekatwa
• Bamia – 10, zimekatwa
• Hoho (bell pepper) – 1, imekatwa
• Cream ya maziwa – ⅓ cup (hiari)
• Tui la Nazi – ½ kikombe
Maelekezo
1. Weka mafuta kwenye kikaangio. Ongeza kitunguu na kaanga hadi kiwe laini na rangi ya dhahabu.
2. Ongeza ginger-garlic paste na pika kwa dakika 1.
3. Weka dagaa waliokangwa na koroga vizuri.
4. Ongeza lemon juice na koroga.
5. Weka nyanya na tomato paste, kisha ongeza chumvi, Maggi, na fish masala.
6. Ongeza cream ya maziwa (hiari) au coconut milk, kisha acha ichemke kwa dakika 3.
7. Ongeza karoti na bamia, funika, pika kwa moto mdogo kwa dakika 3.
8. Fungua, koroga, onja chumvi, kisha ongeza hoho.
9. Koroga na pika kwa dakika 2 zaidi. Chakula chako cha Dagaa kipo tayari kuliwa!
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: