BARABARA NYENGINE PAMOJA NA DARAJA KUBWA LAFUNGULIWA, MAHONDA - PANGATUPU
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2025-12-31
Просмотров: 1780
Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wametakiwa kutumia ipasavyo miundombinu ya barabara inayozidi kuimarishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa lengo la kuinua uchumi wa Zanzibar na kuimarisha biashara ndani na nje ya nchi.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ (TAMISEMI), Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa, wakati wa ufunguzi wa Barabara ya Mahonda–Pangatupu pamoja na Daraja la Pangatupu, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mhe. Kitwana amesema ujenzi na uimarishaji wa barabara hiyo una lengo la kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi kwa kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka maeneo ya uzalishaji vijijini kwenda mjini kwa ajili ya biashara. Ameongeza kuwa barabara hiyo itarahisisha shughuli za usafiri na kutoa fursa za ajira, hususan kwa waendesha bodaboda na vyombo vingine vya usafiri.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Ndugu Ali Said Bakari, akitoa taarifa ya kitaalamu, amesema Barabara ya Mahonda–Pangatupu pamoja na Daraja la Pangatupu ina urefu wa kilomita 11.3 na imejengwa kwa kiwango cha lami. Ameeleza kuwa barabara hiyo imewekewa alama mbalimbali za barabarani kwa lengo la kuimarisha usalama wa watumiaji wa barabara na kupunguza ajali.
Naye Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Mhe. Badria Atai Masoud, amewataka wananchi kuepuka kujenga au kufanya biashara katika hifadhi ya barabara, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuipunguzia Serikali gharama zisizo za lazima na kuharakisha utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo.
#Zanzibar
#BarabaraKwaMaendeleo
#KaskaziniUnguja
#Miundombinu
#UchumiZanzibar
#BreakingNews
#TrendingTikTok
#TrendingYouTube
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: