#MAOMBI_YA_USIKU_MTEMBEO
Автор: ROHO M TV 111
Загружено: 2025-12-03
Просмотров: 400
MAOMBI YA USIKU WA MANANE
1. Kuabudu na Kumshukuru Mungu
“Baba Mungu, nakushukuru kwa wema wako, rehema zako na ulinzi wako juu yangu siku nzima. Nakutukuza kwa kuwa wewe ni alfa na omega, mwanzo na mwisho. Asante kwa pumzi ya uhai, afya na neema iliyotosha.”
2. Kuomba Ondoleo la Dhambi
“Bwana Yesu, nisamehe dhambi zangu zote nilizozitenda kwa mawazo, maneno na matendo. Nisafishe kwa damu yako na unifanye kuwa mtakatifu mbele zako. Nipe moyo mpya na roho iliyo tayari kukufuata.”
3. Kuvunja Kila Nira na Kila Kizuizi
“Ninainua maombi dhidi ya kila nguvu za giza zinazonipinga mimi, familia yangu au ndoto zangu. Kwa jina la Yesu Kristo, navunja kila laana, kila hofu, kila kizuizi, na kila mipango ya adui. Kila mlango uliokuwa umefungwa, ufunguliwe sasa kwa jina la Yesu.”
4. Maombi ya Ulinzi
“Bwana, niweke chini ya kivuli cha mabawa yako. Linda nyumba yangu, watoto wangu, kazi yangu na ndoto zangu. Malaika wako waweke ulinzi mlangoni, madirishani na kila upande. Hakuna silaha iliyoundwa dhidi yangu itakayofanikiwa.”
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: