Wafanya biashara Morogoro wachekelea Sikukuu ya Eid Elftri, Kuku waadimika
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2024-04-09
Просмотров: 228
Wakati waamini wa Dini ya Kiislam kote nchi kesho wakitarajia kushehekea Skukuu ya Eid Elftri, baadhi ya wafanya biashara wa Soko kuu la Chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro wameeleza kufurahishwa na namna walivyofanya biashara kipindi hiki cha Maandalizi ya Skukuu.
Mwananchi Digita imefika kwenye soko kuu la Chifu Kimgalu na kuzungumza na wafanya biashara mbalimbali ambao wameeleza namna walivyofanya biashara zao huku wakisema kuwa Siku kuu hii biashara imefanyika tofauti na Siku kuu zingine huku wengine wakilia hali ngumu.
kwa Upande wake Lukia Ally Muuza kuku kwenye soko kuu la Chifu Kingalu amesema katika biashara yake ya kuuza Kuku, kipindi hiki wameadimika hali inayomfanya ashindwe cha kufanya kwakua alitegemea kuuza kuku kwa wingi kipindi hiki.
(Imeandaliwa na Johnson James)
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: