MALORI 120 HUBEBA MAKAA YA MAWE KWA SIKU JITEGEMEE MBINGA
Автор: KUSINI NEWS
Загружено: 2024-08-14
Просмотров: 1118
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimewatembelea wawekezaji wazawa katika Mkoa wa Ruvuma lengo likiwa ni kampeni ya kuhamasisha uwekezaji na kusajiri biashara zao.
Felix John ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka TIC amesema wapo Mkoani Ruvuma wakitekeleza kampeni ya uhamasishaji uwekezaji wa ndani ambapo wametembelea miradi miwili ya wawekezaji wazawa wa ndani ya Mkoa wa Ruvuma. Moja ya miradi waliotembelea ni Uchimbaji katika Mgodi wa Makaa ya Mawe J wa Kampuni ya ITEGEMEE ambapo Meneja Uchumbaji wa kampuni hiyo Bosco Mabena amesema malori zaidi ya 120 hubeba makaa ya mawe kwa siku na kwamba uzalishaji wa madini hayo unafanyika kwa njia za kisasa.
Amesema makaa ya mawe yanayozalishwa kwenye mgodi wa JITEGEMEE hutumika katika viwanda vilivyopo ndani ya nchi,Afrika Mashariki na nchi za Ulaya na China
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: