#NJOMBE
Автор: Kings FM Digital
Загружено: 2023-05-24
Просмотров: 9318
Mwanaume mmoja mkoani Njombe ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi anatuhumiwa kwa kuwafanyia ukatili wanawake watatu kwa kuwabaka na kuwaingilia kinyume na maumbile kwa zaidi ya wiki moja.
Akizungumza na wananchi wa Kihesa, Halmashauri ya mji Njombe, Mkuu wa Wilaya ya Njombe na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Kissa Gwakisa Kasongwa amesema kuwa Serikali wilayani Njombe inasikitishwa na tukio hilo.
Prisca Mgaya ni Shuhuda namba moja wa tukio hilo na mkazi wa Kilimani eneo la Kihesa hapa anaeleza kile kilichojiri baada ya wananchi kufika kumkamata mtuhumiwa ambapo amesema nguvu za wananchi ndio zilizofanya mtuhumiwa huyo kukamatwa.
Mtuhumiwa wa tukio hilo na waathirika bado wanahojiwa na jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: