MVUA KUBWA YA UPEPO YASABABISHA ATHARI KILOSA MOROGORO; DC SHAKA ASEMA SERIKALI INAFANYA TATHMINI
Автор: Mwl Kyombo
Загружено: 2025-12-27
Просмотров: 10
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliyonyesha usiku wa kuamkia Ijumaa Disemba 26, 2025 wilayani Kilosa Mkoani Morogoro imesababisha athari kwa wakazi wa kata mbili za Dumila na Magole ikiwa ni pamoja na nyumba za makazi na biashara kuathiriwa pamoja na baadhi ya miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na baadhi ya taa za barabarani.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka ametembelea maeneo yalioathirika na mvua hizo na kujionea hali ilivyo na amebainisha kuwa serikali inafanya tathmini ya haraka ili kujua athari zilizojitokeza.
Amefafanua kuwa zaidi ya nyumba 120 zikiwemo za makazi pamoja na maghala mawili ya kuhifadhia nafaka yamekumbwa na maafa hayo.
Aidha amesema kuwa mpaka sasa hakuna athari ya kibinadamu iliyojitokeza kutokana na upepo huo huku akitoa wito kwa wananchi wote wa Kilosa kuchukua taadhari kipindi hiki cha mvua.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: