Gambo Atoa Tuhuma Nzito za Ufisadi wa Mabilioni Ujenzi Arusha, Spika Aingilia Kati,Waziri Atoa Neno
Автор: The Chanzo
Загружено: 2025-04-16
Просмотров: 2013
Dodoma: Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo ameiomba Serikali kutuma timu kwenda kuangalia ujenzi wa jengo la utawala lenye ‘floor’ nane, linalojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 9, jambo ambalo linatia mashaka.
Gambo amezungumza haya leo bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia hotuba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2025/26
“Maana yake kila ‘floor’ moja ni bilioni moja kitu ambacho kwa akili ya kawaida hakiwezekani,” Gambo amesema.
Spika wa Bunge Tulia Ackson amesema kwa uzito wa tuhuma hizo, waziri wa TAMISEMI atakapomaliza hotuba yake atapaswa kuleta taarifa ndogo ya ujenzi wa jengo hilo.
Akijibu, Waziri wa TAMISEMI Mohammed Mchengerwa amekiri kupokea maelekezo hayo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: