RC MBONI MHITA APONGEZA USHIRIKI WA SHINYANGA MAONESHO YA 49 YA SABASABA 2025.
Автор: RS Shinyanga
Загружено: 2025-08-27
Просмотров: 120
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amepongeza ushiriki wa Mkoa wa Shinyanga katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa.
Akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Shinyanga , RC Mhita alisema kuwa ushiriki wa mwaka huu umeonesha ubunifu, mshikamano na jitihada kubwa kutoka kwa taasisi, halmashauri na wajasiriamali wa Mkoa wa Shinyanga.
Amesema mkoa umeendelea kung’ara kwa kuonesha bidhaa bora, huduma za kijamii, pamoja na fursa za uwekezaji zinazopatikana mkoani humo, jambo linalowavutia wageni mbalimbali kutembelea banda la Shinyanga.
Alisisitiza kuwa maonesho hayo ni jukwaa muhimu kwa mkoa kujitangaza, kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na kujifunza kutoka kwa mikoa mingine.
RC Mhita aliwataka washiriki wote waliowakilisha Shinyanga kutumia uzoefu walioupata Sabasaba kuendeleza bidhaa na huduma zao kwa ubora zaidi ili kuvutia masoko ya ndani na nje ya nchi.
Alieleza kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kuwaunga mkono wajasiriamali wadogo na wafanya biashara wakubwa ili waweze kunufaika kiuchumi na biashara wanazofanya ambapo lengo ni kuona wafanyabiashara wote wanainuka kiuchumi hususan kuuza bidhaa zao nje ya nchi.
Kwa ujumla, ushiriki wa Shinyanga mwaka huu umebeba taswira chanya ya maendeleo, ubunifu wa vijana, na jitihada za kukuza uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo, biashara, na huduma.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: