TUTAZAME KULE MBELE — ASUBUHI INAKUJA — NYIMBO ZA WOKOVU N°181 | Swahili Worship Hymns
Автор: Swahili Worship Hymns
Загружено: 2025-12-30
Просмотров: 9756
Tutazame kule mbele,
asubuhi inakuja!
Tuamini Mungu wetu,
atafanya kazi yake,
kufukuza mashetani,
kumiliki nchi yote.
Tutashinda tukiomba,
Mungu anatusikiiya.
Tarumbeta linalia,
tuamke wote sasa!
Mungu wetu anataka
sisi sote tutakaswe!
Kila mmtu awe safi,
Katika kanisa lake!
Uliache nunguniko,
utapata nguvu yake!
Imba ninyi, watu wake,
Bwana yu pamoja nasi!
Tutashinda majaribu
kwa uwezo wake Yesu.
Twende tumhudumie
kwa kumpa mali yake;
hata roho na akili
zimtumikiye Bwana!
Watu wengi hawajui
njia ya kufika mbingu,
wanakuwa wamefungwa
kwa mikono ya shetani.
Twende tukawatafute,
tuwavute kwa Mwokozi,
na kuomba na kukesha
hata kuja kwake Yesu!
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: