MASJID RIDHIWAN MIKUNGUNI KUJENGWA WA GHOROFA, WAFADHILI NA WAUMINI WAPONGEZWA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2025-12-26
Просмотров: 497
Muumini wa Msikiti wa Ridhiwan Mikunguni, Wilaya ya Mjini, Kassim Ameir, amewapongeza waumini wa dini ya Kiislam pamoja na wafadhili mbalimbali kwa kujitokeza kutoa michango ya ujenzi wa msikiti huo.
Akizungumza na Asam Online TV, Kassim Ameir amesema zoezi la ukusanyaji wa michango halikuwa rahisi, kutokana na changamoto ya baadhi ya watu kutokuwa na imani na mchakato wa ukusanyaji wa fedha hizo. Hata hivyo, ameeleza kuwa juhudi, uvumilivu na mshikamano wa waumini umefanikisha lengo hilo muhimu.
Amebainisha kuwa jumla ya fedha zilizofanikiwa kuchangishwa kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Ridhiwan Mikunguni zimefikia shilingi milioni 114, hatua aliyoieleza kuwa ni ushahidi wa mshikamano na mapenzi mema miongoni mwa waumini na wadau wa maendeleo ya dini.
Aidha, ametoa wito kwa waumini kuendelea kushikamana na kudumisha uaminifu ili kukamilisha ujenzi wa msikiti huo kwa manufaa ya jamii na vizazi vijavyo.
#MsikitiRidhiwan
#MchangoWaMaendeleo
#UmojaNaMshikamano
#DiniYaKiislam
#AsamOnlineTV
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: