GARI YA ZIMAMOTO YAPIGWA MAWE NA WANANCHI SHINYANGA | DC & RPC WAONGEA SABABU ZA GARI KUCHELEWA
Автор: Jambo FM Radio Tanzania
Загружено: 2025-11-19
Просмотров: 4900
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kudhibiti fujo zilizofanywa na baadhi ya wakazi katika eneo la Mnara wa Voda lililopo katika halmashuri ya manispaa ya Shinyanga kwa kuliponda mawe gari la zima moto kufuatia kuchelewa kwa gari hilo kufika baada ya kutokea kwa tukio la kuungua kwa nyumba iliyopo katika eneo hilo ambayo mmiliki wake bado hajatambulika mara moja.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amewaonba wananchi kufuata sheria za nchi na kuainisha kuwa kufanya matendo kama hayo ni kosa la jinai hivyo jamii inatakiwa kuchukua tahadhari.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ambaye pia mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro amekemea tabia hiyo huku akiwataka wananchi kuwa na utulivu pindi yanapotokea majanga.
Habari na mwandishi wetu Eunice Kanumba, kutoka 92.7 Shinyanga.
#jambofmtz #chaguamaishafresh
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: