Kilimo cha Azolla Tanzania |Punguza gharama ya malisho ya mifugo tumia AZOLLA|
Автор: Shamba Darasa TV
Загружено: 2022-09-29
Просмотров: 2313
JINSI YA KUZALISHA AZOLLA KWA CHAKULA CHA KUKU
Habari Ndugu Mfugaji popote pale ulipo, jifunze jinsi ya kuzalisha azolla kwa chakula cha kuku na Mkulimastar.
.
Kwa maeneo mengi sana hapa nchini imekuwa changamoto hupatikanaji pamoja na bei za vyakula vya kuku, na watu wengi wamekuwa wakipata wakati mgumu na kufanya ufugaji kuwa na changamoto nyingi na hata kuhahirisha kufanya ufugaji.
Bali sasa vitambue vyakula ambavyo mfugaji unaweza zalisha katika mazingira yake kwa lengo la kulisha kuku wake.
Vifuatavyo ni vyanzo vya chakula ambavyo vyaweza tumika kulisha kuku.
MMEA WA AZOLA.
Huu ni mmea ambao hukua ndani ya muda mfupi na uweza lisha mfugo wako wa kuku na kuwapatia chanzo kizuri cha protini pamoja na viini lishe vinginevyo.
MAZINGIRA YA UZALISHAJI
Eneo ambalo litatumika hakikisha lina funikwa vyema kuweza zuia upotevu mkubwa wa maji, na kuchanganyana na uchafu wa ain ayeyote.
Eneo lisiwe na shughuli nyingine kuepuka kuchanganyikana na uchafu mwingine pamoja na sumu zingine.
Jinsi ya kuotesha.
1. Andaa bwawa square mita 18 kina futi 1.5 au chombo chochote chenye ukubwa wowote unao endana na ukubwa wa eneo ulilo nalo.
2. Kisha weka nailoni ngumu au turubahi ambalo lituzuia kupotea kwa maji Kunywea chinina Baada ya hapo weka samadi udongo kilo 27-30 mbichi ya ng`ombe ambayo itachukua eneo la inchi 10, ondoa uchafu wote hutakao jitokeza baada ya kuweka samadi juu ya maji hayo.
3. kisha weka mbegu kiasi cha kilo tatu (3), katika bwawa hilo maalumu.
4. Baada ya azola kuota Subiri kuvuna baada ya siku 15 kwa Mara ya kwanza baada ya hapo utakuwa ukivuna kila baada ya siku 2-3 kwa zaidi ya mwaka anza kuvuna na kuwapatia kuku wako, baada ya hapo anza kulisha kulingana na wingi wa mifugo ulio nao.
NAMNA YA KUWALISHA.
Kuna namna mbili kuu za kuwalisha kuku,
1. Namna ya kwanza kwa kuwapatia kwa kuchanganya na vyakula vingine kwa kuweka azolla kilo 50, pumba kilo 25, na kilo 25 za chakula cha madukani/ ulichochanganya mwenyewe ili kupata kilo 100
2. Namna ya pili kwa kuwapatia Chakula cha Azolla tu bila chakula kingine.
CHUO CHA MIPANGO
2) AZOLLA
KILIMO CHA CHAKULA BORA CHA MIFUGO KINACHOKUA NA KUVUNWA KILA BAADA YA SIKU (3) TATU TU
Kwetu utapata:
Elimu na utaalam wake
Vitalu vyakuhamishika vyakulimia Azolla (Growbed)
Kuandaliwa bwawa la azolla
Mbegu bora ya Azolla
Bidhaa zake (Vyakula vya mifugo)
LIMA AZOLLA
UPUNGUZE GHARAMA ZA KULISHA MIFUGO YAKO NA UPATE MATOKEO BORA ZAIDI
Azolla ni mmea ambao umethibitika kuwa Chakula bora kwa mifugo na cha gharama nafuu kwani ni mmea rahisi kulima,wenye kutumia eneo dogo na hukua haraka nakuvunwa kila baada ya siku 2-3 tu. Chakula hiki kipo kwenye mfumo wa majani na huwa na virutubisho kwa wingi vya Protini, Vitamins A & B12, amino asidi pamoja na madini mbalimbali ya Calcium, Potassium, Magnesium, Phosphorous na mengineyo mengi.
Chakula hiki cha Azolla huwezakutumika kulisha mifugo mbalimbali kama vile kuku wa Kienyeji, Broilers,Layers, Kuroiler, Malawi, Sasso pia mifugo mingine Kama Bata, Ng'ombe, Nguruwe, Mbuzi, Kondoo, Farasi, Sungura na pia ni chakula kizuri sana kwa Samaki wanaofugwa kwenye mabwawa kama Kambale (Afican Catfish), Sato (Tilapia)n.k
BAADHI YA FAIDA ZA KULISHA AZOLLA KWA MIFUGO YAKO.
1) Kupunguza gharama za chakula kwa mifugo yako kati ya 20% Haswa wafugaji wa kuku wakisasa.
2)Azolla kwa kuku inawasaidia kuongeza kiasi cha utagaji wa mayai na mayai huwa na ubora kwa kuwa na kiini cha njano.
3) Husaidia kupunguza kiasi cha mafuta kwa Ng'ombe na hupelekea kuongeza kiasi cha maziwa kwa Ng'ombe kuanzia 15% -25% na maziwa hayo huwa na ubora wa hali ya juu. ( Low butterfatty)
4) Vile vile inasaidia kupunguza magonjwa kwa mifugo kama Ng'ombe kwa kupunguza magonjwa ya Kimea ambayo huathiri kiwanda cha maziwa kwa Ng'ombe ( Chuchu za Ng'ombe)
5) Azolla pia inasaidia kujenga afya nzuri kwa mifugo yote inayotumia AZOLLA.
6) Ni chakula rahisi kumeng’enywa na mifumo ya chakula ya wanyama aina zote.
7)Huchangia kwenye ukuaji wa haraka wa mifugo mbalimbali.
8) Mbali na Faida kwa mifugo pia Azolla ni mbolea nzuri kwa ajili ya kilimo cha Mbogamboga na mazao mengineyo.
#mkulimasmart
#shambadarasa
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: