MWAKA 2026 MUNGU ATAJIBU MAOMBI YAKO, HATA YALE AMBAYO HUJAYATOA KWA MIDOMO YAKO
Автор: MITIMINGI ONLINE TV
Загружено: 2026-01-10
Просмотров: 99
MWAKA 2026 MUNGU ATAJIBU MAOMBI YAKO, HATA YALE AMBAYO HUJAYATOA KWA MIDOMO YAKO
Waefeso 3:20
“Basi atukuzwe Yeye awezaye kufanya mambo makuu mno, kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.”
Katika mwaka 2026, tarajia Mungu kufanya mambo makubwa sana.
Si tu kwa maombi, bali hata kwa yale hujawahi kuyaomba, hujayawaza, wala hujayajua.
Mungu wetu ana uwezo wa kushangaza, uwezo wa kuinua, uwezo wa kufungua milango ambayo binadamu hawezi kuifungua.
Anaweza kukutendea mambo ambayo akili ya kibinadamu haifiki kwa sababu Yeye ni Mungu wa miujiza isiyo na mipaka.
Mwaka huu 2026
Bwana akupe kuona wema Wake, rehema Zake na kibali Chake. Akutendee mambo makuu sana, hata yale ambayo hujawahi kuyawaza, wala kuyaota.
Kumbuka:
Kuna mambo tunayoyatamani yatokee maishani mwetu, lakini bila Mungu hakuna jambo linaloweza kusimama. Yusufu alipitia mateso, chuki, usaliti, na hata gerezani lakini wakati wa Mungu ulipofika, kutoka gerezani hadi ikulu ilikuwa ni jambo la dakika chache tu. Hivyo ndivyo Mungu anavyoweza kufanya katika maisha yako.
Wana WCC, mwaka 2026 kuna mambo ambayo hatuwezi kwa nguvu zetu. Tunamhitaji Mzee wa Siku Mungu Mwenye Enzi atuingilie kati. Mungu wa Yusufu bado yupo; anaweza kutuma watu toka gerezani hadi ikulu ili jina lake litukuzwe. Kuna wakati Mungu atawachanganya (confuse) watu na mipango yao ili kukuondoa kwenye jaribu na kukupeleka kwenye utukufu.Amini, shika neno, pokea muujiza wako katika jina la Yesu!
Huu ndio mwaka wako wa kuona utukufu wa Mungu ukifunuliwa juu yako na juu ya WCC.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: