MAFANIKIO SEKTA YA AFYA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA LINDI
Автор: Wizara ya Afya Tanzania
Загружено: 2025-10-27
Просмотров: 28
LIGULA RRH: MTWARA KUCHELE YA MATUMAINI MAPYA
Kutoka bahari ya Hindi hadi milima ya Tandahimba, upepo mpya unavuma. Ni upepo wa mabadiliko, wa afya bora, wa matumaini mapya. Ligula Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara, sasa ni alama ya kuamka kwa Kusini. Hapa, ‘Mtwara Kuchele’ si mzaha tena ni alama ya uthabiti, uvumilivu, na ushindi wa wananchi wanaoamini katika nguvu ya kupona.”
Hii ni hadithi ya mji wa bahari, upepo wa korosho, na mioyo yenye ukarimu, kwa muda mrefu, jina “Mtwara Kuchele” lilitamkwa kwa mzaha, kama ishara ya kusubiri maendeleo. Lakini leo, kauli hiyo imepata maana mpya, Mtwara Kuchele kwa ustawi, afya na matumaini mapya.
Chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara – Ligula RRH– imegeuka kuwa kioo cha mabadiliko na kimbilio la matumaini kwa wananchi wa Kusini. Ndoto ya huduma bora za afya haipo tena mbali; sasa inapatikana hapa nyumbani, Ligula.
Majengo mapya yameinuka, vifaa vya kisasa vimeingia, na huduma za kibingwa zimeongezeka; Wagonjwa wanapona kwa wakati; Madaktari wanahudumia kwa weledi na upendo. Kila kona ya hospitali hii inasema kwa sauti moja: “Afya bora inawezekana, hapa Mtwara.”
Ligula RRH ni ushahidi halisi wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kujenga Taifa lenye afya bora, usawa na heshima kwa utu wa binadamu. Kutoka Mtwara iliyokuwa inasubiri, hadi Mtwara inayoongoza hii ndiyo hadithi ya Ligula, hadithi ya mabadiliko, matumaini, na uzima wa kizazi kipya.
Fuatana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, kwenye makala hii maalum yenye simulizi za watumishi wa afya, wagonjwa, na wananchi wa Mtwara, wakishuhudia kwa maneno na matendo namna Mtwara Kuchele sasa imekuwa Mtwara ya mafanikio.
@ikulu_mawasiliano @samia_suluhu_hassan @gersonmsigwa @maelezonews @who
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: