CBE Dodoma ilivyozindua Awamu ya 3 ya Mafunzo kwa Wahudumu wa Mabasi ya Masafa Marefu!
Автор: CBE DODOMA CAMPUS
Загружено: 2025-06-05
Просмотров: 285
UZINDUZI AWAMU YA TATU YA MAFUNZO KWA WAHUDUMU WA MABASI YA MASAFA MAREFU
Tarehe 26 Mei 2025, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma kimezindua rasmi awamu ya tatu ya mafunzo kwa wahudumu wa mabasi ya masafa marefu, yakifunguliwa na Mkurugenzi wa Kampasi hiyo – Prof. Kembo Bwana.
Prof. Kembo aliambatana na viongozi kampasi wa chuo wakiwemo:
Dkt. Josephine Churk – Meneja wa Taaluma, Tafiti na Ushauri wa Kitaalamu
Dkt. Liberatus Gabagambi – Meneja wa Mipango, Fedha na Utawala
Dkt. Adrian Ndunguru – Mratibu wa Mafunzo hayo kwa Kampasi ya Dodoma
Prof. Kembo alieleza kuwa wahudumu hao wataendelea kupata semina mbalimbali kutoka LATRA, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Huduma ya Kwanza (First Aid) – kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa huduma salama, za heshima na zenye weledi kwa abiria.
“Tunawakaribisha kuwa mabalozi wa CBE. Chuo hiki kinatoa pia kozi za muda mrefu katika ngazi mbalimbali – kuanzia Certificate, Diploma, Bachelor hadi Masters.” – Prof. Kembo Bwana
Hongera kwa wahudumu wote walioanza safari hii ya maarifa! Hiki ni kielelezo cha dhamira ya CBE katika kukuza sekta ya usafirishaji kupitia elimu bora na ya vitendo.
@cbe.dodoma
#CBE #DodomaCampus #MafunzoKwaWahudumu #MasafaMarefu #LATRA #UsafiriSalama #JeshiLaPolisi #Zimamoto #HudumaYaKwanza #VyuoVikuuTanzania #ElimuNiNguvu #TransportTraining #CBE2025
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: