Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu, RC Morogoro atoa wito.
Автор: RS MOROGORO
Загружено: 2025-12-03
Просмотров: 140
Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu, RC Morogoro atoa wito.
Leo Disemba 3, 2025 yamefanyika maadhimisho ya siku ya watu wenye Ulemavu kitaifa hapa katika Manispaa ya Morogoro huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Kighoma Malima ambaye ametumia fursa ya maadhimisho hayo kuzitaka Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya kwa kundi la watu wenye ulemavu.
Akibainisha zaidi Mhe. Malima amesema, kumekuwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa ngazi ya halmashauri kutotenga fedha kwa ajili ya watu wenye ulemavu na kuwataka kutenga fedha hizo kwa sababu kundi hilo lina haki sawa na watu wengine huku akisema fedha hizo zitawasaidia kupata vifaa tiba vitakavyowasaidia.
Aidha, Mhe. Malima amesema Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeendelea kujali kundi hilo, ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/25 kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 238 kilitolewa kwa vyama 13 na Shirikisho la SHIVYAWATA.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kutunza amani, kwani amani ikitoweka wahanga wakubwa ni watu wenye ulemavu. Hivyo ni jukumu la kila mmoja kuendelea kuilinda amani ya Tanzania kwa wivu mkubwa.
“Tunahitaji amani; sisi walemavu hatuwezi kukimbia,” amesisitiza Mhe. Adam Malima.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum,Wakili Amon MpanjuMhe. Amon Mpanju, amewataka viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali, washawishi wa mitandao, wasanii na viongozi wa siasa kutumia majukwaa yao kuhubiri amani kwa kuwa ndio nguzo ya Taifa.
Naye Bw. Hamadi Abdallah, akimwakilisha Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), amesema Serikali haina budi kufanya mapitio ya Sera inayohusu Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, kuzindua mwongozo wa huduma za afya kwa watu wenye ulemavu na mwongozo wa taifa wa ufikivu, ambayo yatachagiza ujenzi wa jamii jumuishi ya watu wenye ulemavu.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Kuendeleza jamii jumuishi kwa watu wenye ulemavu: mstakabali wa ustawi wa jamii.”
Mwisho.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: