MELI KUTOKA IRAN YATIA NANGA BANDARI YA TANGA
Автор: Tanga Tanzania TV
Загружено: 2025-11-30
Просмотров: 190
TANGA: BANDARI ya Tanga imezidi kufunguka kutokana na kupokea meli za mizigo kwa wingi ambapo MV Parnia yenye mizigo ya makasha 463 kutoka Iran imetia nanga.
Hatua hiyo ni sehemu ya uwekezaji uliofanywa na serikali kwa ujenzi wa gati sambamba na ununuzi wa vifaa vya kisasa vya upakuaji wa shehena za mizigo, hivyo kuongeza ufanisi kwenye bandari hiyo.
Akizungumza wakati wa upokeaji wa meli hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Burian aliwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya ujio wa meli hiyo, kuhakikisha inarudi na shehena ya mzigo kutoka nchini.
“Wafanyabiashara wa katani, mazao ya viungo sambamba na kahawa ni fursa kwenu kupeleka bidhaa hizo nchini Iran, kwani kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa hizo,” alisema.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: