Elimu ya uanzishaji wa chama cha ushirika kwa maafisa usafirishaji wa Kasulu - Kigoma
Автор: LatraTV
Загружено: 2025-07-15
Просмотров: 187
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imetoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Usafirishaji wa Pikipiki za Magurudumu Mawili Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma katika ukumbi wa shule ya Sekondari Bogwe, Juni 21, 2025.
Akizungumza katika Mkutano huo ulioratibiwa na Mhe. Prof. Joyce Ndalichako Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, Bw. Vumilia Simbaye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, ameipogeza LATRA kwa kutoa elimu hiyo kwa Maafisa Usafirishaji hao kwani wakianzisha ushirika utaenda kukuza uchumi wao.
Naye Bw. Salum Pazzy Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano LATRA, amewaeleza maafisa usafirishaji hao fursa na faida watakazo zipata pale watakapo anzisha chama chao cha ushirika kwani LATRA imeweka mazingira wezeshi kwa maafisa kuanzisha vyama vyao vya ushirika.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mhe. Prof. Joyce Ndalichako Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, ACP Damas Patrick Mkuu wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kasulu, Bw. Ado Msigala Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Kigoma, Ibrahim Katenza Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu pamoja na Maafisa Usafirishaji wa Pikipiki za Magurudumu Mawili Wilayani humo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: