Vodacom Tanzania PLC yazindua kampeni kubwa ya kitaifa inayobeba ujumbe wa “Tupo Nawe,Tena na Tena.”
Автор: Kajunason TV
Загружено: 2025-06-10
Просмотров: 78
Katika kuadhimisha miaka 25 ya kuwaunganisha Watanzania, Vodacom Tanzania PLC imezindua kampeni kubwa ya kitaifa inayobeba ujumbe wa “Tupo Nawe, Tena na Tena.” Kampeni hii itakayodumu kwa miezi minne, kuanzia Juni hadi Oktoba 2025, inalenga kusherehekea safari ya mafanikio tangu walipoanza kutoa huduma nchini mnamo mwaka 2000 hadi leo.
Vodacom inawakumbusha Watanzania kuwa ipo nao sambamba katika kila hatua ya maisha yao, kutoka kipindi cha mawasiliano ya simu za kawaida hadi zama hizi za dijitali za M-Pesa, 5G, huduma za afya mtandaoni, elimu kwa njia ya simu na biashara za kidijitali.
"Miaka 25 ya Vodacom siyo tu kuhusu teknolojia; ni kuhusu mahusiano tuliyojenga na maisha ya Watanzania tuliyoyagusa. Kupitia ‘Tupo Nawe, Tena na Tena,’ tunawashukuru Watanzania kwa kutuamini na kutufanya kuwa mtandao wa mawasiliano unaoaminiwa na watu wengi zaidi nchini. Hali kadhalika, tunawaahidi kuwa bado tupo na tutaendelea kuwa nanyi kwa miaka mingi ijayo," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Philip Besiimire.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: