Onyo Rasmi! Polisi Wawaka Hasira kwa Wanaosambaza Maudhui ya Kuchochea Mitandaoni
Автор: GREEN FM TV
Загружено: 2025-10-05
Просмотров: 48
Jeshi la Polisi Tanzania limeonya vikali dhidi ya tabia ya baadhi ya watu kutumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kusambaza maandishi, picha na picha za mjongeo zenye lengo la kuchochea vitendo vya kihalifu vinavyokwenda kinyume na maadili, utamaduni wa Mtanzania na sheria za nchi.
Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, imeelezwa kuwa vitendo hivyo vya kihalifu vinavyosukumwa na dhamira ovu, licha ya kuwa ni kinyume cha sheria, vimekuwa vikisababisha hofu na taharuki kwa wananchi wema wasiokuwa na hatia yoyote.
“Tabia hizo na vitendo hivyo vinapaswa kukemewa na kupigwa vita na kila Mtanzania anayejua umuhimu na thamani ya amani kwa maisha yake na familia yake,” imeeleza taarifa
Aidha Jeshi la Polisi limewahakikishia wananchi kuwa linaendelea na juhudi za kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote wanaohusika na matumizi hayo mabaya ya mitandao, na tayari baadhi yao wameshakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Pia Jeshi hilo limewaonya wale ambao bado wanaendelea na vitendo hivyo kuwa wasijidanganye, kwani kinachosubiriwa ni muda tu pamoja na ukamilishaji wa taratibu za kisheria ili wafikishwe katika vyombo vya haki kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: