WATOTO WA MIAKA 5 WAPONA ULEMAVU BAADA YA MSAADA WA WORLD VISION NA CCBRT
Автор: Makutano TV
Загружено: 2022-08-14
Просмотров: 600
Ester Timoth Mapunda na Winfrida Christopher Mwenda ni watoto wenye umri wa miaka mitano, watoto hawa wakiwa katika hatua ya ukuaji walipata changamoto iliyopelekea ulemavu, baada ya kupatiwa msaada wa utengamao kupitia shirika lisilo lakiserikali la World vision watoto hawa wamepona.
Katika Makala hii tunaangazia mchango wa asasi za kiraia katik kumlinda mtoto na kuleta haki na ustawi wa mtoto, World Vision Tanzania katika Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Serikali wameweza kujenga miundo mbinu kwa watoto wenye ulemavu, na kutoa kadi za bima ya afya kwa Zaidi ya watoto 400.
Tupo katika kijiji cha Ikungwe na Muwimbi Iringa vijijini na hapa ndipo watoto Ester na Winifrida wanaendelea na maisha yao kama kawaida bada ya muujiza wa mponyaji, wazazi wanasimulia Furaha yao ya kupona kwa watoto hawa
Mtaalamu wa tiba kwa vitendo na mratibu wa huduma za vitimwendo CCRBT Moshi, Bi Neophita Lukiringi anasema miongoni mwa sababu zinazoweza kupelekea mtoto kupata ulemavu ni pamoja na ukosefu wa chakula bora wakati wa ukuaji wa mtoto, kuumia kwa ubongo mtoto anapozaliwa kunakotokana na mama kuchelewa kujifungua ama baada ya kuzaliwa kama atapata homa kali au kuanguka na kuumia ubongo
Msimamizi wa watoto kutoka World vision anazungumza namna walivyotambua watoto hawana na ufuatiliaji uliofanyika
Kwa mujibu wa mwongozo wa Taifa wa utambuzi wa mapema na afya stahiki kwa watoto wenye ulemavu unaeleza kuwa tafiti zinaonyesha ulemavu unaweza kuzuilika kwa asilimia 80, pia imedhihirika kuwa utambuzi wa mapema wa ulemavu kwa mtoto unaweza kupunguza makali na athari za ulemavu ukubwani na katika Makala hii tumeona utambuzi wa mapema umesaidia mtoto Ester na Winfrida kuweza kupona.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: