NYANGUKU WAMPA JINA LA FAHARI ENG CHACHA ‘’NZAGAMBA’’ – AFAFANUA… “NIKO TAYARI KWENDA KUPIGANA”
Автор: MwangazaTV
Загружено: 2025-10-16
Просмотров: 79
#mwangazatvupdates
Katika hali iliyojaa matumaini makubwa, wakazi wa Kata ya Nyanguku wamempa jina la heshima “Nzagamba” mgombea ubunge wa Jimbo la Geita Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Eng. Chacha Wambura.
Jina hilo, ambalo kwa asili hutumiwa kwa ng’ombe dume wa heshima mwenye hadhi ya kipekee katika jamii nyingi za mikoa ya Kati na Magharibi mwa Tanzania, linaashiria nguvu, ujasiri, na uongozi wa kweli.
Jina hilo hutolewa kwa anayejitokeza mbele ya wengine kwa kujiamini, kupambana bila woga na kulinda maslahi ya kundi lake, Katika Mkutano wa Kampeni wananchi wa Kata ya Nyanguku walimvisha Eng. Chacha shuka la heshima na kumtaja rasmi kuwa “Nzagamba”
Akizungumza mara baada ya kutunukiwa jina hilo, Eng. Chacha Wambura alitoa hotuba ya kugusa mioyo ya wengi na kwa sauti ya kujiamini, aksimema amepokea jina hilo kwa mikono miwili na yuko tayari kwenda kupigana kwa ajili ya maendeleo ya jimbo la Geita Mjini.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: