MAJINA YASIYOSTAHIKI KWA WATU WENYE ULEMAVU
Автор: ZENJI UPDATE
Загружено: 2025-12-03
Просмотров: 23
Mpenzi Mfuatiliaji wa Zenji update youtube chanal karibu katika Makala safi kabisa inayozungumzia Athari za majina yasiyostahiki kwa watu wenye ulemavu ni kukujuza tu kwamba ni mimi mtayarishaji wa Tatu Juma kuwa nami mwanzo hadi tamati ya Makala hiki.Wakati Dunia ikiadhimisha siku ya watu wenye ulemavu leo hii Disemba 3 ndugu mfuatiliaji Mada hii imejikita hasa katika kupinga matumizi ya majina yasiyofaa au yenye kejeli yanayoathiri taswira, heshima,na nafasi ya watu wenye ulemavu.
Malengo mahsusi nikuelekeza majina yasiyostahiki yanayotumika kwa watu wenye ulemavu napia kuelewa taswira hasi inayojitokeza kutokana na matumizi ya majina hayo na kueleza athari za kijamii na kisaikologia zinzowakumba watu wenye ulemavu kutokana na lugha hiyo
.Pia kuwahimiza matumizi ya lugha jumuishi yenye heshima ili kukuza usawa na utu kwa watu wote na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kubadili mitazamo hasi na kukuza staha katika mawasiliano.Mbali na hayo pia kwaupande wa sheria ya watu wenye ulemavu Zanzibar namba 8 ya mwaka 2022 kifungu namba 30 kinaeleza kwamba kila mtu anawajibu wa kutekeleza,kulinda na kutetea haki za watu wenye ulemavu ukijumuisha kutoa taarifa zinazohusiana na uvunjwaji wa haki hizi. ambapo kifungu 31 [1] kinazungumza kuwa watu wenye ulemavu hawatobaguliwa au kudhalilishwa kwa namna yeyote ile na katika ngazi zote kutokana na sababu ya ulemavu wao.
Ndugu mpenzi Mfuatiliaji Leo hii nipo na Khamis Zahor mkaaazi wa Makadara ambae anaulemavu wa viungo Pamoja na Seif Salim Said mkaazi wa Meya Mjini Unguja wakieleza kwahisia kali jinsi wanavyochoshwa na kuathirika kisaikologia juu ya uitwaji wa majina yasiyostshiki.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: