KAMANDA MULIRO USO KWA USO NA MAAFISA USAFIRISHAJI AKITOA TAMKO KUPINGA TAARIZA ZA KICHOCHEZI
Автор: Mtanzania Digital
Загружено: 2025-10-18
Просмотров: 1028
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amewataka Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) kutojihusisha na mambo yanayoweza kuleta taharuki.
Kamanda Muliro ameyasema hayo leo Oktoba 18, 2025 wakati akizungumza na Maafisa hao katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala wilayani Temeke.
Muliro amesema "Tumefanya kikao na Maafisa Usafirishaji, tumewakumbusha kujiepusha na vitendo viovu na kutojiingiza katika mambo mbalimbali yanayoweza kuleta taharuki ili wawe na fursa nzuri yakufanya shughuli zao za usafirishaji ambazo kimsingi wale watakaozingatia misingi ya kisheria na ubora wa kazi hii wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo mazuri na baadae kusonga mbele kutoka kwenye kazi ya juu zaidi ya usafirishaji"
Kwa upande wake Filimoni Laiser Afisa usafirishaji maeneo ya Mbagala Temeke amelishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wao kwa kukubali kusikiliza kero zao na kuahidi kuzifanyia Kazi. Hivyo wanategemea kufanya kazi zao kwa Amani na Utulivu na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Jeshi la Polisi hasa katika upande wa usalama ili kufanya Mbagala na Jiji la Dar es salaam kwa ujumla kuwa shwari.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: