Shabiki ataka Aishi Manula aongezwe kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya AFCON 2025
Автор: Azam TV
Загружено: 2025-12-13
Просмотров: 153
AFCON 2025: “Wachezaji wazuri wameitwa ila kidogo nilikuwa napendekeza kwa kocha, Aishi Manula angemuongeza”
Shabiki wa soka anayeishi Tabata Mwananchi Dar es Salaam, anasema kundi ambalo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ipo sio jepesi na Watanzania wampe muda Kocha Miguel Gamondi.
Shabiki huyo anasema anaheshimu maamuzi ya Kocha Gamondi, lakini anashauri kuongezwa kikosini kwa golikipa Aishi Manula.
‘Mwamba’ huyo ambaye anasema yeye na pacha wake ni mafundi wa ‘boli’ na yeye anaweza akapiga nafasi ya Anthony Mligo au hata ya Mohamed Hussein.
Shabiki mwingine anasema Taifa Stars itarudi na kombe na ameonesha namna atashangilia kombe likitua Tanzania.
Michuano ya #AFCON2025 itaanza kutimua vumbi Desemba 21, na mechi zote 52 zitakuwa LIVE katika kisimbuzi cha #AzamTV
#AFCON2025
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: