Learn KiSwahili with a Story | Simba na Panya
Автор: Kiswahili ni Urithi
Загружено: 2024-02-17
Просмотров: 71
Hadithi, hadithi.... hadithi njoo, ukweli njoo, utamu kolea...
Siku moja Simba alikuwa amelala karibu na mti.Juu ya ule mti, kulikuwa na panya mmoja. Panya aliteleza kwa bahati mbaya akamdondokea Simba kichwani. Simba akamkamata. Akamwambia, kwa nini umenikanyaga? Leo nitakula nyama yako.
Panya akasema, ninaomba unisamehe.
Ni bahati mbaya. Ukinisamehe, na mimi nitakusaidia siku nyingine. Basi, Simba akamsamehe. Panya akaenda zake.
Siku chache baadaye, Simba alinaswa kwenye mtego wa mwindaji. Akaanza kunguruma ili kuomba msaada. Panya alisikia mngurumo wa Simba. Akakimbia kwenda kumsaidia. Panya akakatakata ule mtego kwa meno yake. Simba akatoka. Simba alimshukuru sana Panya kwa kumwokoa.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: